Kupitia kwa msemaji wa klabu Haji Manara, klabu imetangaza rasmi tarehe za matukio makubwa yanayoenda kufanyika hivi karibuni, Wiki Ya Mwananchi Pamoja na uzinduzi wa jezi mpya za msimu wa 2022/23.
“Wiki ya Wananchi itaanza rasmi tarehe 1 moja mwezi wa 8 na kilele chake kitakuwa tarehe 6, Itakuwa ni wiki ya kipekee na itamuwa special na bora sana kuliko zote zilizopita, Mwisho kabisa tuko tayari kwa maandalizi ya msimu ujao” alisema Haji Manara akiongea na waandishi wa habari mapema leo.
Kuhusu uzinduzi wa jezi, Haji alidokezea kuwa uzinduzi utafanyika wiki ijayo.
“Mungu akitujalia wiki ijayo tutazindua jezi mpya za msimu ujao kwa klabu yetu”, Haji Manara.