Wachezaji wameanza program ya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2022/23.
Baadhi ya wachezaji waliokuwa sehemu ya mazoezi hayo ni wachezaji wetu wageni ; Lazarous Kambole, Gael Bigirimana, Lomalisa Mutambala, na Aziz Ki. Huku baadhi ya wachezaji wetu wengine wakiwa kwenye majukumu yao ya timu ya taifa.
Yanga inaendelea kujidhatiti vyema kwenye kambi ya Avic Town -Kigamboni.