KUHUSU KLABU
Young Africans Sports Club, maarufu kama YANGA ni klabu ya michezo iliyoanzishwa Februari 11, 1935. Makao makuu yetu ni Jangwani, Dar Es Salaam, Tanzania na uwanja wetu wa nyumbani ni Benjamin Mkapa.
Klabu yetu ina timu 4 tofauti zinazoshiriki mashindano tofauti yanayotambulika na Shirikisho la soka Tanzania ‘TFF’. Tuna timu kubwa ya Wanaume, Timu mbili za vijana chini ya miaka 20 na 17. Tuna timu ya Wanawake inayotambulika kama Yanga Princess.
Timu yetu kubwa ya wanaume imetwaa makombe 28 ya Ligi Kuu Tanzania Bara, makombe 2 ya AZAM FEDERATION CUP, Washindi mara 7 wa Ngao ya Jamii na Ubingwa mara 5 wa CECAFA.
Yanga ni klabu kongwe zaidi Tanzania yenye wafuasi wengi zaidi Afrika Mashariki na Kati.