• Young Africans Sports Club
MPYA
  1. YANGA YAFUZU KWA KISHINDO, YAICHAPA VITAL’O 6-0
  2. MATCH DAY! SIKU YA KIHISTORIA IMEFIKA
  3. WACHEZAJI WAPO TAYARI KUIKABILI VITAL’O
  4. GAMONDI : NINA TIMU BORA
  5. USAJILI WANACHAMA KIDIJITALI ZAMU YA KAGERA

Young Africans Sports Club maarufu kwa jina la Yanga, ilisajiliwa rasmi na Mamlaka za serikali Februari 11, 1935, lakini historia rasmi ya klabu ya Yanga ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1920, wakati vijana wa eneo la Dar es Salaam walipokuwa wakikusanyika kwenye viwanja vya Jangwani kwa shughuli za michezo.

Vijana hao walianzisha timu ya mpira iliyoitwa Jangwani Boys, na mwaka 1926 kulifanyika mkutano wa wadau wote wa Jangwani Boys iliyokuwa imepata umaarufu mkubwa.

Kwenye mkutano huo vijana wa Jangwani Boys walimchangua Tabu Mangala, kuwa Mwenyekiti wa timu hiyo. Tabu Mangala alikuwa na ushawishi mkubwa kwa wafanyakazi wa Bandari ambao waliijiita jina la Talian.

Mkutano huo pia ulikubaliana kubadili jina kwa kuziunganisha Talian na Jangwani Boys na kuiita klabu ya Navigation hasa baada ya ushawishi mkubwa wa watu waliokuwa wafanyakazi wa Bandari.

Jina la Navigation halikudumu sana baada ya Hayati Abeid Aman Karume kuona jina hilo halileti maana waliyoikusudia hivyo wakati wa mwaliko wa Pasaka Viwani Zanzibar timu ilirejea Dar es Salaam na kubadili jina na kuitwa New Youngs 1930.

New Youngs ilizidi kuwa kubwa na kuvuta hisia za watu wengi, wakiwemo wanasiasa waliokuwa wakipambania Uhuru, hivyo maskani ya New Youngs ilikuwa inawakutanisha vijana, wazee na watu wengine mashuhuri,

Vijana walikusanyika kwa michezo na Watu mashuhuri na wazee walikusanyika kwa shughuli maalumu za kupanga mipango ya kutafuta Uhuru wa Tanganyika.

Ilipofika mwaka 1935, Yanga ilisajiliwa rasmi kwa jila na Young Africans Sports Club. Neno ‘Africans’ likaleta hisia tofauti kwenye masuala ya kisiasa hivyo baadhi ya watu waliogopa masuala ya Siasa waliamua kujitenga mwaka 1936.

Kundi hili la waliojitenga hasa wenye asili ya Asia walikwenda kuanzisha timu yao na Yanga ikabaki kwa wananchi wa kawaida.

Wakati Yanga ilipoamua kuchukua uelekeo wa kisiasa timu haikufanya vizuri kwenye michezo jambo ambalo lilianza kuleta mgawanyiko kwa baadhi ya watu kuamini siasa inawakwamisha kwenye mafanikio ya mpira.

Lakini uongozi wa Yanga ulisimama imara na baadae mafanikio yakaanza kwa timu kubeba makombe kwenye mashindano waliyokuwa wakishiriki. Huu ukawa mwanzo wa utawala wa Yanga kwenye mpira wa Tanzania.

MABADILIKO YA UENDESHAJI WA KLABU (2020 -)

Mwaka 2020, uongozi wa Yanga ulitia saini mkataba wa ushauri  wa uendeshaji wa timu kwa mfumo wa kisasa na kampuni ya La Liga inayosimamia Ligi Kuu soka nchini Hispania.

Mei 27, mwaka huo,wanachama wa klabu walikubali kubadilisha muundo wa uongozi wa klabu ili kuruhusu wawekezaji kuingia kwenye uendeshaji wa timu.

Miaka miwili baadae, Julai 9, 2022 baada ya mabadiliko ya uendeshaji kufanyika, wanachama wa Yanga walipiga kura kwenye mkutano mkuu wa klabu na kumchagua Eng. Hersi Said kuwa Rais wa kwanza wa Yanga, kwenye historia ya klabu hiyo.

2020-
MIAKA YA MABADILIKO
- Taji la Ligi Kuu - Ngao Ya Hisani - Azam FA Cup
2010's
- Ligi Kuu X 5 (2010–11, 2012–13, 2014–15, 2015–16, 2016–17, 2021–22) - FA Cup X 2 (2015–16, 2021/22) - Ngao ya Hisani X 5 (2013, 2014, 2015, 2021, 2010) - CECAFA X 2 (2011, 2012)
2000's
- Ligi Kuu Tanzania Bara x 6 (2002, 2005, 2006, 2007–08, 2008–09,) - Tusker Cup x 2 (2007, 2009) - Mapinduzi Cup X 1 (2004) - Community Shield X 2 (2001,)
1990's
- Tanzania Premier League x 6 (1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998) - Tanzania FA Cup x 2 (1994, 1999) - CECAFA Cup x 2 (1993, 1999,) - Kwa mara ya kwanza tumefika kwenye hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika. (1998)
1980's
- Tanzania Premier League: x 5 (1981, 1983, 1985,1987, 1989)
1970's
- Tanzania Premier League: x 4 (1970, 1971, 1972, 1974) - Tanzania FA Cup: x 1 (1975) - CECAFA: x1 (1975)
1960's
- Baada ya Ligi Kuu Tanzania bara kuanzishwa mwaka 1965, Yanga ilichukua ubingwa wake wa kwanza mwaka 1968 na kushinda mfululizo kwa miaka mitano. - Kushiriki kwa mara ya kwanza Klabu Bingwa Afrika Mafanikio: Tanzania Premier League: X 2 (1968, 1969)
1930's
Kuundwa kwa klabu ya Dar Young Africans Sports Club
- Ilipofika mwaka 1935, Yanga ilisajiliwa rasmi kwa jila na Young Africans Sports Club na ikawa tishio sana, neno Africans likaleta hisia tofauti kwenye masuala ya kisiasa hivyo watu wengine waliiogopa masuala ya Siasa waliamua kujitenga mwaka 1936 na kutokea timu mbili, baadhi ya watu hasa wenye asili ya Asia walikwenda kunzisha timu yao, na Yanga ikabaki na Wazawa.

Main Sponsor